array(0) { } Radio Maisha | Joseph Ole Lenku kuchunguzwa kwa madai ya ufujaji wa fedha

Joseph Ole Lenku kuchunguzwa kwa madai ya ufujaji wa fedha

Joseph Ole Lenku kuchunguzwa kwa madai ya ufujaji wa fedha

Tume ya Kukabili Ufisadi, EACC imetakiwa kumchunguza Gavana wa Kajiado, Joseph Ole Lenku kwa madai ya ufujaji wa fedha za umma.

Mbunge wa Kajiado ya Kati, Elijah Memusi amesema Lenku alitumia shilingi milioni 22 kufanikisha hafla ya kuonesha mafanikio yake kwenye mwaka wa kifedha uliopita maafuru Lenku Report Card.

Aidha Memusi anasema tangu aliposhika hatamu za uongozi agosti tarehe nane mwaka wa 2017, Gavana Lenku amenunua mashamba yenye thamani ya shilingi zaidi ya milioni sabini katika maeneo ya Kajiado Kusini na Loordokilani.

Hata hivyo gavana huyo amekana madai hayo akisema yu tayari kuchunguzwa na iwapo atapatikana na hatia ashtakiwe kwa mujibu wa sheria.

Lenku aidha amesema hakutumia shilingi milioni 22 kuainisha mafanikio yake Ijumaa wiki iliyopita, akisema serikali yake haina fedha za kutumia katika hafla za kaunti.

Hata hivyo amesema alitumia chini ya shilingi laki tano kununua chakula na kuwalipa waimbaji waliowatumbuiza wageni siku hiyo.