array(0) { } Radio Maisha | Vijana watakiwa kufuata sheria kilifi kuhusu mauaji ya wazee.

Vijana watakiwa kufuata sheria kilifi kuhusu mauaji ya wazee.

Vijana watakiwa kufuata sheria kilifi kuhusu mauaji ya wazee.

Vijana kwenye kaunti ya Kilifi wametakiwa kufuata sheria wakati wanapotafuta suluhu ya masuala ya wazee kuuliwa kiholela kwa madai ya uchawi.

Kwa mujibu wa Mwakilishi wa Wadi ya Garashi Peter Ziro, japo idadi ya visa hivyo vimepungua kwa kiasi kikubwa bado kuna maeneo ambapo vimekithiri hasa eneo bunge la Magarini akidai kuwa visa hivyo huchochewa na vijana wanaodaiwa kuungana na kuwaangamiza wazee hao akionya kuwa hatua hiyo ni kinyume na sheria.

Wakati uo huo mwakilishi huyo amewataka wanafunzi na wakazi kwa jumla kuwa makini wakati huu wa likizo ili kupunguza visa vya mimba za mapema pia visa vya uhalifu ambavyo hukithiri wakati huu.

Aidha amewaonya wazazi dhidi ya kusuluhisa kesi za mimba za mapema nje ya mahakama akisisitiza haja ya kuwasilisha kesi hizo mahakamani, akidai hatua hiyo imechangia kuongezeka kwa kesi hizo katika jamii.

Ikumbukwe mwaka jana takwimu zilizotolewa na Wizara ya afya na ile vijana katika kaunti hiyo, zilibainisha zaidi ya visa elfu kumi na saba vya mimba za mapema katika kaunti hiyo, huku wengi wa walioathirika wakiwa wanafunzi ambao asilimia kubwa walilazimika kusitisha masomo yao.