array(0) { } Radio Maisha | Mkenya mmoja miongoni mwa watano ameshindwa kulipa mkopo wa Benki au mikopo kupitia simu

Mkenya mmoja miongoni mwa watano ameshindwa kulipa mkopo wa Benki au mikopo kupitia simu

Mkenya mmoja miongoni mwa watano ameshindwa kulipa mkopo wa Benki au mikopo kupitia simu

Utafiti uliofanywa na Shirika la Financial Sector Deepening unaonesha kuwa Mkenya mmoja miongoni mwa watano ameshindwa kulipa mkopo kati mwaka mmoja uliopita.

Utafiti huo unaonesha kuwa kudorora kwa uchumi kumewaathiri sana Wakenya hasa wakulima. Aidha kwa mujibu wa utafiti huo, wengi hukopa kutoka benki au mashirika ya mikopo kulipia madeni waliyo nayo.

Ripoti ya Benki Kuu ya Kenya, CBK inaonesha kuwa kufikia mwezi Mei, takriban shilingi trilioni 2.7 ni mikopo ya Benki ambayo haijalipwa huku bilioni 430.1 ikiwa mikopo ya watu binafsi.

Vilevile madeni yanayokopwa kwa simu mfano Tala, Branch, Okash imepata umaarufu sana kutokana na urahisi wa kupewa mikopo.