array(0) { } Radio Maisha | Magoha kuongoza kongamano la CBC hapo kesho

Magoha kuongoza kongamano la CBC hapo kesho

Magoha kuongoza kongamano la CBC hapo kesho

Waziri wa Elimu, Profesa George Magoha kwa sasa anatathmini mikakati ya maandalizi ya Kongamano la Mtalaa wa Umilisi CBC katika ukumbi wa KICC, ambapo amesema kwamba serikali i tayari kufanikisha utekelezaji wa mtalaa huo.

Kongamano hilo la kitaifa litaanza rasmi hapo kesho likiwaleta pamoja washikadau mbalimbali kujadili hatua ambazo zimepigwa hadi sasa kufanikisha utekelezaji wake.

Waziri Magoha aidha amesema serikali imetenga mgao wa kutosha kufanikisha mchakato huo na kwamba kongamano hilo litatoa fursa kwa washikadu mbalimbali kujadili masuala yanayohusu CBC.

Kangamano hili linajiri wakati ambapo baadhi ya washikadau kikiwamo Chama cha Kitaifa cha Walimu, KNUT wakisisitiza kwamba serikali haijaweka mikakati  ya kufanikisha shughuli hiyo na kwamba imeharakishwa.