array(0) { } Radio Maisha | Githu Muigai aunga mkono katiba kufanyiwa marekebisho

Githu Muigai aunga mkono katiba kufanyiwa marekebisho

Githu Muigai aunga mkono katiba kufanyiwa marekebisho

Aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Githu Muigai ameunga mkono suala la katiba kufanyiwa marekebisho akisema kwamba gharama ya kusimamia shughuli za serikali imeongezeka.

Muigai amesema kuwa serikali imeshindwa kumudu hali ya maisha ya Wakenya na kwamba pana haja ya marekebishao ya katiba. Vilevile amesema sehemu ya 6 ya katiba inastahili kuangaizwa upya ili kubuniwa kwa serikali ndogo ambayo itaweza kusimamia mahitaji ya wananchi pasi na matatizo.

Akizungumza katika kongamano la mawakili linaloendelea jijini Mombasa, Muigai amependekeza kuondolewa kwa makamishana na majukumu yao kujumuishwa katika wizara mbalimbali.

Wakati uo huo, amesema wakati umefika kwa serikali kuhamia katika mfumo utakaojumuisha uongozi wa wote kulinganisha na mfumo wa sasa ambao ameutaja kuwa wa kuongoza na kugawanya.