array(0) { } Radio Maisha | Jopo la majaji 3 kuzuru KICC kukagua sanamu ya Jomo Kenyatta

Jopo la majaji 3 kuzuru KICC kukagua sanamu ya Jomo Kenyatta

Jopo la majaji 3 kuzuru KICC kukagua sanamu ya Jomo Kenyatta

Jopo la majaji watatu wa Mahakama Kuu wakati wowote kuanzia sasa, linatarajiwa kuzuru Jumba la KICC jijini Nairobi ambako sanamu ya Rais wa kwanza wa Kenya Jomo Kenyatta ipo.

Ziara ya majaji hao inalenga kuthibitisha iwapo sanamu hiyo ni sawa na iliyo kwenye noti mpya zinazoendelea kutumika nchini.

Ikumbukwe kuwa mwanaharakati Okiya Omtatah  aliwasilisha kesi kupinga kutumiwa kwa noti hizo kwa msingi kwamba zina picha ya Hayati Jomo Kenyatta kinyume na matakwa ya kifungu cha 231 ibara ya nne ambayo inasisitiza kwamba noti za Kenya hazipaswi kuwa na sura ya mtu yeyote.