array(0) { } Radio Maisha | Mombasa: taharuki yatanda katika eneo la Soko Mjinga Mtongwe Likoni

Mombasa: taharuki yatanda katika eneo la Soko Mjinga Mtongwe Likoni

Mombasa: taharuki yatanda katika eneo la Soko Mjinga Mtongwe Likoni

Hali ya taharuki inaendelea kutanda katika eneo la Soko Mjinga Mtongwe Likoni kwenye Kaunti ya Mombasa kufuatia hatua ya maafisa wa jeshi la KDF wa Kambi ya Mtongwe, Naval Base kuendelea kuwashambulia watu kwa siku ya pili mfululizo baada ya mwenzao kuuliwa.

Wakazi wanadai maafisa hao wamekuwa wakitembea katika kundi la watu wanane katika maeneo tofauti na kumpiga yeyote wanayekutana naye.

Idadi ya watu waliojeruhiwa haijulikani kufikia sasa huku wakazi wa eneo hilo wakiendelea kuishi kwa hofu.

 

Shughuli za kawaida eneo hilo zikiwamo za usafiri na biashara zimetatizika kufuatia uvamizi wa maafisa hao.

Usiku wa kuamkia jana watu kadhaa wakiwamo maafisa wawili mmoja wa Kitengo cha Polisi wa Utawala na mwingine wa Kitengo cha Huduma za Wanyamapori, KWS walikuwa walijeruhiwa baada ya kupata kichapo cha mbwa kutoka kwa maafisa hao.

Uvamizi wa maafisa hao unatajwa kuwa wa kulipiza kisasi baada ya mwenzao kuuliwa kwa kuchomwa siku tano zilizopita.

Jana kamishna wa Likoni Joseph Lenkara amesema kwamba tayari wamewasiliana na wakuu wa kambi ya Naval Base ambao waahidi kuhakikisha suala hilo linachunguzwa kwa mara moja.