array(0) { } Radio Maisha | ODM kuchagua atakaye wania kiti cha Ubunge Kibra

ODM kuchagua atakaye wania kiti cha Ubunge Kibra

ODM kuchagua atakaye wania kiti cha Ubunge Kibra

Chama cha ODM kimesema kingali kinashauriana kuhusu ni nani kitakachomchagua kupeperusha bendera yake katika uchaguzi mdogo wa Eneo Bunge la Kibra.

Katibu Mkuu wa ODM, Edwin Sifuna amesema kwamba wiki ijayo, Baraza Kuu la Chama cha ODM litakutana kujadili suala hilo, huku akiwaomba wakazi wa Kibra kuwa na Subra.

Haya yanajiri siku moja tu baada ya Spika wa Bunge la Kitaifa, Justin Muturi kukitangaza kuwa wazi kiti hicho, huku Tume Huru ya Uchaguzi na Uratibu wa Mipaka IEBC, ikisubiriwa kutangaza tarehe ya uchaguzi.

Ikumbukwe kulingana na sheria IEBC ina siku tisini baada ya kiti cha ubunge kutangazwa kuwa wazi, kuandaa uchaguzi mdogo.

Kiti hicho cha Kibra kilisalia wazi kufuatia kifo cha aliyekuwa Mbunge wa eneo hilo, Ken Okoth tarehe 26 mwezi Julai mwaka huu.