array(0) { } Radio Maisha | Maraga aagiza kubuniwe kamati za upatanisho zitakazo suluhisha mzozo baina ya Seneti na Bunge la Kitaifa

Maraga aagiza kubuniwe kamati za upatanisho zitakazo suluhisha mzozo baina ya Seneti na Bunge la Kitaifa

Maraga aagiza kubuniwe kamati za upatanisho zitakazo suluhisha mzozo baina ya Seneti na Bunge la Kitaifa

 

Spika wa Bunge la Seneti, Ken Lusaka ameagizwa kubuni kamati ya upatanisho ambayo itashirikiana na kamati sawa na hiyo ya Bunge la Kitaifa kusuluhisha mvutano wa muda kuhusu kiwango cha fedha kinachostahili kutengewa serikali za kaunti.

Akitoa agizo hilo, Jaji Mkuu David Maraga amesema kamati hizo mbili zina jukumu la kuafikiana ili kuhakikisha kwamba shughuli na huduma katika kaunti zinaendelea bila mwananchi kuathirika na kuongeza kwamba kesi hiyo itasikilizwa tarehe 16 mwezi ujao.

Awali, maspika wa Bunge la Kitaifa - Justin Muturi na mwenzake wa Seneti, Ken Lusaka kupitia mawakili wao, wameieleza mahakama kwamba wameshauriana jinsi walivyoagizwa na mahakama iyo hiyo mwezi uliopita na kuwa mpango wa mashauriano umepiga hatua. Profesa Kithure Kindiki  anaiwakilisha Seneti katika kesi hiyo.

Akiunga mkono kauli hiyo, wakili wa Baraza la Magavana - Fred Ngatia amesema mvutano unaoendelea baina ya Bunge la Kitaifa, Seneti, Mamlaka ya Ugavi wa Mapato na Serikali za kaunti sio tu kuhusu fedha, bali pia ukosefu wa maafikiano kuhusu mwelekeo wa kisheria.

Amesiitiza kauli yake ya awali kwamba ni mahakama hiyo tu ndiyo yenye mamlaka ya kutoa mwelekeo.

Ikumbukwe kuwa serikali za kaunti zinashinikiza kuongezwa kima cha shilingi bilioni 19 ili kufanikisha utendakazi wake.

Vikao hivyo vilihudhuriwa na wawakilishi wa Baraza la Magavana, Mamlaka ya Ugavi wa Mapato CRA, Msimamizi wa Bajeti na maafisa wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.