array(0) { } Radio Maisha | Mombasa: Idara ya usalama kuwachukuliahatua wazazi wanaowatelekeza watoto.

Mombasa: Idara ya usalama kuwachukuliahatua wazazi wanaowatelekeza watoto.

Mombasa: Idara ya usalama kuwachukuliahatua wazazi wanaowatelekeza watoto.

Idara ya usalama katika Eneo Bunge la Changamwe imeonya kuwa itawachukulia hatua kali wazazi wanaowatelekeza watoto wao.

Onyo hili limetolwa baada ya kubainika kwamba baadhi yao wamekuwa na tabia ya kuwachia walimu majukumu ya ulezi, ilihali ni jukumu la wazazi kukaa na watoto wao na kuwafunza maadili hususan wakati huu wa likizo.

Naibu Kamishna wa eneo hilo, Tom Onyelo amewataka wazazi kuwajibika katika ulezi wa wanao huku akionya kuwachukulia hatua kali vijana wanaowahangaisha wananchi katika mitaa ya Changamwe.