array(0) { } Radio Maisha | TSC yalaumiwa kwa mvutano wa KNUT
TSC yalaumiwa kwa mvutano wa KNUT

Naibu Mwenyekiti wa Kitaifa  wa Chama cha Walimu Nchini, KNUT Collins Oyuu amedai mvutano unaoshuhudiwa chamani humo umesababishwa na Tume ya Huduma kwa Walimu, TSC.

Akiwahutubia wanahabari mjini Nyamira, Oyuu amewashauri viongozi wa chama hicho kukumbatia ushirikiano katika shughuli za utekelezaji wa majukumu yao ili kufanikisha ajenda za chama hicho.

Oyuu vilevile amesema viongozi wa  KNUT wako tayari kushiriki mazungumzo na TSC ili kuafikia mwafaka kuhusu hatua ya TSC kufeli kutuma michango ya walimu ya kila mwezi kwa chama hicho hali inayokisiwa kuwa mbinu ya kutaka kulemaza utendakazi wa KNUT.

Ameyasema haya wakati baadhi ya viongozi wa KNUT wa eneo la Kati ya Nchi wamemtaka Katibu Mkuu wa KNUT, Wilson Sossion kung'atuka katika uongozi wa chama hicho.