array(0) { } Radio Maisha | KCB yarekodi faida ya shlingi bilioni 12.7

KCB yarekodi faida ya shlingi bilioni 12.7

KCB yarekodi faida ya shlingi bilioni 12.7

Benki ya Kenya Comercial imerekodi kuongezeka kwa faida yake kwa asilimia 5 zikiwa ni shilingi bilioni 12.7 katika kipindi cha nusu mwaka kilichokamilika mwezi Juni.

Akizungumza alipotangaza faida hiyo Meneja Mkurugenzi wa Benki hiyo Joshua Oigara amesema mapato hayo yamechangiwa na kuongezeka kwa idadi ya wateja wake wanaotumia mpango wa kuomba mkopo kupitia simu KCB M-Pesa.

Wakati uo huo amesifia uwekezaji wa benki hiyo, ambao amesema umechangia katika ukuaji wa matawi yake, kote nchini.