array(0) { } Radio Maisha | Wadhifa wa ubunge wa Kibra watangazwa kuwa wazi
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

Wadhifa wa ubunge wa Kibra watangazwa kuwa wazi

Wadhifa wa ubunge wa Kibra watangazwa kuwa wazi

Na Victor Mulama,

NAIROBI, KENYA, Spika wa Bunge la Kitaifa Justin Muturi ametangaza rasmi wadhifa wa ubunge wa Kibra kuwa wazi kufuatia kifo cha aliyekuwa Mbunge wa eneo hilo Ken Okoth tarehe 26 mwezi Julai mwaka huu.

Muturi ameiagiza Tume ya Uchaguzi, IEBC kuandaa uchagzui wa kumtafuta mbunge wa eneo hilo ndani ya kipindi cha siku tisini.

Tangazo hili linajiri wakati ambapo tayari ushindani mkali umeibuka miongoni mwa wandani wa Kiongozi wa Chama cha ODM Raila Odinga ambao wanaolenga kutwaa wadhifa huo.

Miongoni mwa wanaotarajiwa kuwania wadhifa huo kupitia tiketi ya chama cha ODM ni Imran Okoth ambaye ni ndugu ya marehemu, aliyekuwa msaidizi wa Raila Eluid Owalo, aliyekuwa Mbunge wa Embakasi Kusini Irshad Sumra, aliyekuwa Seneta Elizabeth Ongoro, Kiongonzi wa Vijana kwenye chama hicho, Benson Musungu na Katibu Mkuu wa ODM, Edwin Sifuna.

Kwa mujibu wa katiba, wadhifa wa mbunge anayefariki dunia akiwa ofisini unapaswa kutangazwa siku ishirini na moja baada ya siku yake ya kufariki.