array(0) { } Radio Maisha | Mzozo mwingine walikumba Kanisa la Kiadventista
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

Mzozo mwingine walikumba Kanisa la Kiadventista

Mzozo mwingine walikumba Kanisa la Kiadventista

Na Carren Papai

NAIROBI, KENYA, Mzozo baina ya makundi mawili yanayozozana kuhusu uongozi wa Kanisa la Kiadventista la Maxwel Central jijini Nairobi unazidi kutokota huku kundi moja likiwataka viongozi wote wa kanisa hilo kujiuzulu ili kupisha uongozi mpya.

Kundi hilo limekanusha taarifa kwamba linazozania shilingi milioni ishirini na tano jinsi ilivyodaiwa awali, na badala yake kushikilia kwamba ni mabilioni ya pesa yamepotea kutokana na usimamizi mbaya wa mali ya kanisa hilo.

Kundi hilo limesema waanzilishi wa kanisa hilo walitoa mali yao kwa hiari ili kuendeleza shughuli za kidini hali ambayo imeathiriwa na uongozi mbaya.

Kanisa hilo la Maxwel SDA , lilifungwa na maafisa wa Polisi baada ya kuwatawanya waumini ambao walikuwa wakizozana kanisani humu siku ya Jumapili iliyopita.