array(0) { } Radio Maisha | OCS wa Kizingitini, Lamu alikamatwa kimakosa
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

OCS wa Kizingitini, Lamu alikamatwa kimakosa

OCS wa Kizingitini, Lamu alikamatwa kimakosa

Na Caren Omae

NAIROBI, KENYA, Siku chache tu baada ya kukamatwa kwa Mkuu wa Polisi wa Kituo cha Kizingitini - Lamu, Shadrack Mumo pamoja na maafisa watatu wa polisi kwa madai ya kumwachilia mshukiwa wa ulanguzi wa dawa za kulevya, sasa imebainika alikamatwa kinyume na sheria.

Inaarifiwa mnamo tarehe kumi na moja, maafisa wa polisi waliokuwa wakishika doria walifika nyumbani kwa mshukiwa kisha kupata dawa kadhaa za kulevya ila mshukiwa mwenyewe akafanikiwa kutoroka.

Hata hivyo, maafisa hao walifika kituoni na dawa hizo kisha kurekodi taarifa. Mwendo wa saa nne usiku tarehe iyo hiyo, Kamanda wa Polisi eneo la Lamu Muchangi Kioi akazungumza na Mumo kuhusu tukio hilo.

Aidha, baadaye Kamanda aliwatuma polisi kumkamata usiku huo ilhali hakuwa katika eneo la tukio wakati wa msako.

Inaarifiwa baada ya Kioi kugundua kwamba alikuwa ameagiza kunaswa kwa Mumo pamoja maafisa hao kinyume na sheria, akawasiliana na wakuu wa kituo alichozuiliwa ili kufunguliwa mashtaka ya utovu wa nidhamu.

Jumanne jioni, Ipara alimwagiza Kamanda wa Polisi wa Kituo hicho kumwachilia Mumo ila akakataa huku akitaka kufikishwa mahakamani kesho ili kufunguliwa mashtaka.

Mumo tayari amewaagiza mawakili wake kuwasilisha kesi mahakamani kumshtaka kamanda huyo wa polisi.