array(0) { } Radio Maisha | Ni wabunge 15 pekee waliosafiri kuelekea Jijini Nashville-Tennessee, Marekani
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

Ni wabunge 15 pekee waliosafiri kuelekea Jijini Nashville-Tennessee, Marekani

Ni wabunge 15 pekee waliosafiri kuelekea Jijini Nashville-Tennessee, Marekani

Na Ether Kirong'

NAIROBI, KENYA, Huku mjadala kuhusu suala la Kenya kuwatuma wajumbe tisini kuhudhuria Kongamano la Wajumbe wa mataifa mbalimbali ukiendelea, sasa wabunge wamesema ni wajumbe kumi na watano pekee waliohudhuria kongamano hilo Jijini Nashville-Tennessee Marekani.

Mbunge mmoja ambaye asingependa kutajwa jina lake, ameiambia Radio Maisha kwamba kumi na watano hao waliwajumuisha wabunge, maseneta na wawakilishi wa wadi.

Mbunge huyo amesema kwa jumla shilingi milioni 100 zilitumika kugharimia safari hiyo. Hata hivyo amepuuza madai kwamba ni wabunge tisa pekee waliohudhuria kongamano hilo huku wengine wakivinjari katika maeneo mbalimbali.

Aidha, akihojiwa katika Runinga ya KTN NEWS, Mbunge wa Homa Bay mjini, Peter Kaluma amesema bunge halipaswi kulaumiwa hasa ikizingatiwa uozo uliosheheni katika idara nyingine serikalini ambapo viongozi wamekuwa wakipanga ziara za ghafla ili kutumia pesa za umma visivyo.

Haya yanajiri huku ripoti ya msimamizi wa bajeti ikionesha kwamba bunge limetumia takriban shilingi bilioni 2.5 kwa ziara za nje katika kipindi cha miezi tisa. Aidha serikali za kaunti zimetumia shilingi bilioni 9.4 kipindi sawa na hicho.

Wizara ya Masuala ya Kigeni imetumia shilingi milioni 801 katika kipindi sawa na hicho. Wizara ya Michezo imetumia shilingi milioni 325.

Aidha Mahakama ya Juu imetumia shilingi milioni 25, afisi ya Mkuu wa Mashtaka ya Umma shilingi milioni 56 huku afisi ya rais ikitumia shilingi milioni 53.