array(0) { } Radio Maisha | Raia wa Nepal waliokamatwa kwa Punjani kushtakiwa

Raia wa Nepal waliokamatwa kwa Punjani kushtakiwa

Raia wa Nepal waliokamatwa kwa Punjani kushtakiwa

Na Carren Omae,

NAIROBI, KENYA, Washukiwa watatu waliokamatwa katika makazi ya mfanyabiashara Ali Punjani anayehusishwa na ulanguzi wa dawa za kulevya wanatarajiwa kufikishwa mahakamani Jumatano.

Watatu hao ambao ni mkewe Punjani, Karki Sushmija na raia wawili wa Nepal na India walihojiwa jana katika Kituo cha Polisi cha Nyali.

Raia wa India alipatikana na msokoto mmoja wa bangi wakati msako ulipokuwa ukiendeshwa katika nyumba ya Punjani.

Ikumbukwe Punjani yuko nchini India kwa matibabu kufuatia maradhi ya moyo. Hata hivyo maafisa wa upelelezi wamemtaka kujiwasilishwa kwao Jumapili wiki ijayo. Aidha Punjani kupitia mawakili wake amesema atarejea nchini tarehe ishirini na sita mwezi huu.