array(0) { } Radio Maisha | Afariki baada ya kushiriki ngono katika shamba la mahindi.

Afariki baada ya kushiriki ngono katika shamba la mahindi.

Afariki baada ya kushiriki ngono katika shamba la mahindi.

Maafisa wa polisi wanachunguza kisa ambapo mwanamume mmoja mwenye umri wa miaka 35 alipatikana hapo jana akiwa ameaga dunia katika Kijiji cha Chepyakwai Kaunti Ndogo ya Kapsaret baada ya kushiriki ngono katika shamba la mahindi.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi katika Kaunti Ndogo ya Kapseret Francis Warui, alipata ripoti kutoka kwa wakaazi wa kijiji hicho kuwa marehemu Julius Bor alikuwa akijistarehesha na mpenziwe Janet Cheruto mwenye umri wa miaka 40 kabla ya kuaga.

Jackson Misoi mzee wa mtaa amesema kuwa wawili hao walikuwa wakivinjari katika shamba la mahindi ambapo Bor alizirai.

Inaaminika mwanamke huyo alijaribu kumpa maji  kisha kumwita mwanawe Bor kumsaidia lakini juhudi zao za kumwokoa ziligonga mwamba.
Hatimaye walipiga ripoti kwa mzee wa mtaa ambaye aliwafahamisha polisi waliofika katika eneo la tukio.

Mwili wa marehemu umelazwa katika hifadhi ya maiti ya Hospitali ya Rufaa ya Moi Mjini Eldoret ukisubiri upasuaji kubaini chanzo kamili cha kifo chake.