array(0) { } Radio Maisha | Watu watatu raia wa Nepal wamekamatwa katika makazi ya Ali Punjani
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

Watu watatu raia wa Nepal wamekamatwa katika makazi ya Ali Punjani

Watu watatu raia wa Nepal wamekamatwa katika makazi ya Ali Punjani

Polisi eneo la Nyali Kaunti ya Mombasa wanaendeleza msako katika nyumba ya mfanyabiashara Ali Punjani anayehusishwa na ulanguzi wa dawa za kulevya.

Maafisa hao wanatumia mbwa wanne wa kunusu kutekeleza msako huo unaoongozwa na Kamanda wa Polisi wa Kaunti ya Mombasa, Johnstone Ipara.

Maafisa wanne walio na mbwa hao wamesambazwa sehemu tofauti za makazi hayo chini ya uangalizi wa Ipara na mawakili wa familia ya mfanyabiashara huyo vilevile jamaa za Punjani.
 
Baadhi ya maafisa ambao wamekuwa wakikita kambi kwenye jengo hilo tangu jana wemevalia sare rasmi na wengine sare kawaida.
 
Hayo yanajiri huku Punjani akiwa nchini India ambako anatibiwa maradhi ya moyo.

Wakati uo huo,

Watu watatu raia wa Nepal wamekamatwa katika makazi ya mfanyabiashara Ali Punjabi eneo la Nyali kwenye Kaunti ya Mombasa.

Watu hao Karki Sushmija kwenye umri wa miaka ishirini na minne, Shira Bashyal na mwanamume mwingine wamekuwa humu nchini kwa muda wa miezi miwili sasa. Alipohojiwa, Karki amesema kwamba ni mke wa Punjani.

Raia hao wanaendelea kuhojiwa na maafisa wa mbalimbali wa idara ya usalama ambao wamekuwa wakiendeleza msako katika makazi ya Punjabi anayedaiwa kuhusishwa na ulanguzi wa mihadarati.