array(0) { } Radio Maisha | Pigo kwa chama cha ODM baada ya Eliud Owalo kujiuzulu
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

Pigo kwa chama cha ODM baada ya Eliud Owalo kujiuzulu

Pigo kwa chama cha ODM baada ya Eliud Owalo kujiuzulu

Aliyekuwa msaidizi wa kinara wa Chama cha ODM, Eliud Owalo amejiuzulu rasmi kutoka chama hicho.

Katika barua aliyomtumia Katibu Mkuu wa ODM - Edwin Sifuna, Owalo amesema kwamba aidiolojia zake na za chama hicho haziambatani na kwamba hana msisimko wa kuwa mwanachama wa ODM ilivyokuwa awali na hivyo kumtaka Sifuna kuliondoa jina lake kutoka sajili ya wanachama wake.

Hata hivyo, inaarifiwa kwamba huenda Owalo ana mipango ya kuhamia Chama cha Amani National Congress ambacho ananuia kuwania wadhifa wa ubunge eneo la Kibra, ulioachwa wazi kufuatia kifo cha Ken Okoth.

Owalo ametajwa kuwa miongoni mwa wanaokimezea mate kiti hicho. Wengine ambao wanatarajiwa kutangaza azma ya kuwania wadhifa huo ni aliyekuwa Mbunge wa Embakasi Kusini Irshad Sumra, aliyekuwa Seneta Elizabeth Ongoro, Kiongonzi wa Vijana kwenye chama hicho Benson Musungu na Katibu Mkuu wa ODM, Edwin Sifuna.

Ushindani huo unajiri wakati Spika wa Bunge la Kitaifa, Justin Muturi Ijumaa wiki hii akitarajiwa kutangaza rasmi wadhifa huo kuwa wazi kufuatia kifo cha Okoth tarehe 26 mwezi Julai mwaka huu.

Karani wa Bunge la Kitaifa, Michael Sialai amedokeza kwamba Muturi atatangaza wadhifa huo kuwa wazi Ijumaa ikizingatiwa kwamba leo ni siku ya kumi na saba tangu kufariki dunia kwa Okoth. Kwa mujibu wa Katiba, wadhifa wa mbunge anayefariki dunia akiwa ofisini unapaswa kutangazwa siku ishirini na moja baada ya siku yake ya kufariki.

Baada ya wadhifa huo kutangazwa kuwa wazi, Tume ya Uchaguzi, IEBC inatarajiwa kuandaa uchaguzi mdogo chini ya kipindi cha miezi mitatu baada ya kupokea notisi rasmi kutoka kwa Muturi.