array(0) { } Radio Maisha | Magoha awashauri wakuu wa vyuo vikuu kutoa mafunzo kuhusu cbc

Magoha awashauri wakuu wa vyuo vikuu kutoa mafunzo kuhusu cbc

Magoha awashauri wakuu wa vyuo vikuu kutoa mafunzo kuhusu cbc

Waziri wa Elimu, Profesa George Magoha amewashauri wakuu wa vyuo vikuu kutoa mafunzo kuhusu Mtalaa wa Umilisi, CBC kwa wanafunzi wanaosomea kozi za ualimu kwa manufaa ya walimu.

Akizungumza katika Chuo Kikuu cha Kenyatta, Waziri Magoha amesema mtalaa huo utafaulu tu iwapo walimu watapata mafunzo ya kutosha.

Aidha, Magoha amesema serikali imetenga fedha za kufanikisha mtalaa huo mpya hivyo walimu wanapaswa kupewa mafunzo ya kutosha. Amewasihi washikadau katika sekta hiyo kushirikiana ili kufanikisha mtalaa huo ambao tayari unapingwa na Chama cha KNUT.

Kwa upande wake, Naibu Mkuu wa chuo hicho, Paul Wainaina, wakuu wa vyuo vikuu watashirikiana na serikali kufanikisha mtalaa huo