array(0) { } Radio Maisha | Owino akana madai kwamba ODM ilididimiza hatua yake kuwa mkuu wa polisi

Owino akana madai kwamba ODM ilididimiza hatua yake kuwa mkuu wa polisi

Owino akana madai kwamba ODM ilididimiza hatua yake kuwa mkuu wa polisi

Kufuatia madai kwamba Chama cha ODM kilididimiza juhudi zake za Msemaji wa Polisi Charles Owino kuwa Mkuu wa Polisi, Owino amekana madai hayo akisema kwamba uteuzi wa nafasi hiyo si wajibu wa upinzani wala chama chochote kile cha siasa.

Katika taarifa mapema leo, Owino amesema kwamba hana kinyongo na  chama hicho wala Kinara wake Raila Odinga.

Hata hivyo, Owino amesema kwamba aliyekuwa Mbunge wa Ugenya Chris Karan,  alimwonya kwamba ODM ingetumia mamlaka yake kusambaratisha azma yake kuwa Mkuu wa Polisi. Owino amesema vitisho hivyo vilitokana na sababu kwamba alidhaniwa kuwa mfuasi wa David Ochieng' mpinzani wa Chris Karani katika uchaguzi mdogo uliondaliwa Ugenya.

Owino amesema anaunga mkono uongozi wa Mkuu wa Polisi Hillary Mutyambai huku akiwataka viongozi wengine kufanya hivyo kwa manufaa ya usalama wa taifa.