array(0) { } Radio Maisha | Polisi wakashifiwa kwa kuwatawanya waumini Jumamosi.

Polisi wakashifiwa kwa kuwatawanya waumini Jumamosi.

Polisi wakashifiwa kwa kuwatawanya waumini Jumamosi.

Idara ya Polisi imekashifiwa na kutakiwa kukoma kutumiwa vibaya baada ya Uongozi wa Kanisa la Kiadventista la Central jijini Nairobi kuiilaumu serikali kwa kuwatawanya waumini Jumamosi wiki iliyopita kwa madai kwamba kulikuwa na agizo la mahakama.

Kwa mujibu wa viongozi wa kanisa hilo, polisi walikiuka haki za waumini waliokuwa kanisani Jumamosi kwa shughuli ya kuabudu.

Aidha, wamemshtumu Kamishna wa Nairobi, Flora Mwoloa kusema kwamba kuna mzozo wa uongozi kanisani humo.

Hata hivyo, viongozi hao wamewahakikishia waumini kwamba kanisa hilo litaendeleza shughuli kama kawaida, vilevile wako tayari kwa mazungumzo ili kupata suluhu.

Waumini waliofika walishauriwa kuifanyia ibada katika shule iliyo karibu ya St. Georges huku malango ya kanisa hiyo yakisalia kufungwa. Makundi hayo mawili yanasemekana kutofautiana kuhusu uongozi wa kanisa hilo. Visa sawa na cha Jumamosi vimekuwa vikishuhudiwa kwa zaidi ya mwezi mmoja sasa.