array(0) { } Radio Maisha | Elam Esendi akamatwa kwa kusaidia kuachiliwa mshukiwa.

Elam Esendi akamatwa kwa kusaidia kuachiliwa mshukiwa.

Elam Esendi akamatwa kwa kusaidia kuachiliwa mshukiwa.

Siku moja tu baada ya Waziri wa Masuala ya Ndani ya Nchi, Fred Matiang'i kuwaonya walanguzi wa dawa za kulevya, afisa wa polisi anayesimamia Kituo cha Kizingitini Kaunti ya Lamu, Elam Esendi pamoja na maafisa wa polisi wamekamatwa kwa kusaidia kuachiliwa kwa mlanguzi wa dawa za kulevya.

Inaarifiwa wanne hao walimwachilia mlanguzi huyo wa mihadarati baada ya kukamatwa jana mjini Lamu kwa kuhusishwa na biashara hiyo haramu. Ikumbukwe Waziri Matiang'i akizungumza jana aliwaonya watu wanaoendesha biashara hiyo kwamba watakabiliwa kwa mujibu wa sheria.

Aidha, akizungumza leo katika Uwanja wa Ronald Ngala jijini Mombasa, Mbunge wa Mvita, Abdhulswamad Sharif ameipongeza hatua ya kukamatwa kwa OCS huyo maafisa wengine watatu wa polisi kwa kumwachilia mshukiwa huyo.

Kauli yake imetiliwa mkazo na aliyekuwa mgombea ugavana wa Kaunti ya Mombasa, Suleiman Shahbal.