array(0) { } Radio Maisha | Roselyne Akombe kutoa ushahidi kuhusu uchaguzi wa mwaka 2017

Roselyne Akombe kutoa ushahidi kuhusu uchaguzi wa mwaka 2017

Roselyne Akombe kutoa ushahidi kuhusu uchaguzi wa mwaka 2017

Huku juhudi za kuwaunganisha wananchi zikiendelea, suala la udanganyifu wakati wa uchaguzi mkuu uliopita huenda likachipuka upya baada ya aliyekuwa Kamishna wa Tume ya Uchaguzi, IEBC Roselyne Akombe kutangaza kwamba yu tayari kutoa ushahidi kuhusu yaliyojiri wakati wa uchaguzi huo wa mwaka 2017.

Akombe ambaye kwa sasa ni mfanyakazi wa Umoja wa Mataifa, ametangaza hili kupitia mtandao wake wa Twitter ambapo vilevile amedai kwamba alikuwa amependekeza kubuniwa kwa jopo maalum la kuchunguza yaliyojiri wakati wa uchaguzi huo ambapo matokeo ya kwanza ya urais yalifutiliwa mbali na Mahakama ya Juu kufuatia visa vya udanganyifu.

Ikumbukwe kuwa Akombe alijiuzulu kutoka wadhifa huo siku kadhaa kabla ya marudio ya uchaguzi huo mwezi Oktoba mwaka 2017 na kuelekea jijini New York baada ya kudai kwamba IEBC haikuwa na uwezo wa kuendesha uchaguzi huo kutokana na uegemeaji wa mirengo wa baadhi ya makamishna wa tume hiyo akiwamo mwenyekiti wake Wafula Chebukati.