array(0) { } Radio Maisha | Watu ishirini na watatu wagunduliwa wakiugua saratani Nairobi.

Watu ishirini na watatu wagunduliwa wakiugua saratani Nairobi.

Watu ishirini na watatu wagunduliwa wakiugua saratani Nairobi.

Jumla ya watu ishirini na watatu waligunduliwa wakiugua saratani kufuatia ukaguzi bila malipo uliofanywa wiki hii katika hospitali ya Mama Lucy na Mbagathi jijini Nairobi. Aidha madaktari wamewashauri  wawili miongoni mwao kufanyiwa uchunguzi zaidi wa kiafua.

Daktari Musa Mohammed ni Mkuu wa Madaktari katika hospitali ya Mama Lucy hata hivyo maafisa wa afya wamesema kwamba waathiriwa wanaweza kushughulikiwa kwani saratani hiyo haijaenea sana. .

Kulingana na takwimu ni kwamba wanawake saba walipatikana wakiugua saratani ya matiti, huku kumi na wawili walipatikana wakiugua saratani ya nia ya uzazi huku mwanaume mmoja akipatikana akiugua saratani ya
korodani yaani Prostrate Cancer. Mohamed Dagane ni Mkurugenzi wa Afya kwenye Kaunti ya Nairobi.

Hayo yanajiri huku serikali ya Kaunti ya Nairobi ikisema hivi karibuni itaanzisha mpango wa kuhamasiha umma kuhusu umuhimu wa kutafuta huduma za afya kwa lengo la kupunguza kuongezeka kwa idadi ya watu wanaougua saratani. Aidha amesena wataimarisha huduma katika hospitali jijini.

Gavana wa Nairobi Mike Sonko amewashauri wakazi kuendelea kuvitembea vituo vya afya kwa ukaguzi wa mara kwa mara ili waweze kutibiwa kwa wakati.

Ukaguzi huo uliendeshwa kwa ushirikiano na Hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta.

Amesema serikali ya kaunti itafanya kazi kwa karibu na washikadau wa sekta ya afya ili kufanikisha kampeni hiyo. Wakati uo huo, inalenga kushirikiana na kaunti zilizo karibu pamoja na serikali kuu kwa ujenzi wa kituo cha uchunguzi na kutoa matibabu dhidi ya saratani jijini.