array(0) { } Radio Maisha | Sukari magunia mia tisa na hamsini imeibwa Mombasa.

Sukari magunia mia tisa na hamsini imeibwa Mombasa.

Sukari magunia mia tisa na hamsini imeibwa Mombasa.

Sukari magunia mia tisa na hamsini iliyo na nembo ya Zambia White Sugar iliyokuwa inahifadhiwa katika eneo la kuhifadhi bidhaa la BENVIC lililo eneo la Owino Uhuru Mombasa imeibwa.

Katika taarifa iliyonakiliwa kwenye Kituo cha Polisi cha Jomvu, takriban watu sihirini waliokuwa wamejihami kwa silaha butu walilivamia eneo hilo na kuwafunga kwa kamba mikononi na miguuni  bawabu wawili wanaolinda eneo hilo kabla kutekeleza wizi huo.

Wezi hao waliyapaikia magunia hayo kwenye gari aina ya Canter kisha kutoweka nayo. Wanadaiwa vile vile kuziharibu Camera za CCTV zilizo eneo hilo kabla kutekeleza uhalifu huo.

Magunia hayo yanadaiwa kuhifadhiwa katika eneo hilo tangu tarehe sita Disemba mwaka jana na mafisa wa Mamlaka ya Ukusanyaji Kodi KRA.

Tukio hio linajiri huku Idara ya Upelelezi DCI ikiendelea kukichunguza kisa cha kuibwa kwa takriban magunia elfu tano ya sukari inayokisiwa kuwa na madini ya zebaki Mercury ambayo ilikuwa inahifadhiwa kwenye eneo la Kuhifadhi bidhaa la Bollore Where house lililo eneo la Changamwe Kwenye Kaunti ya Mombasa.

Kamanda wa Polisi eneo la Changamwe Daudi Loronyoke amesema kwamba wizi huo ulitekelezwa wiki tatu zilizopita na kesi hiyo ikakabidhiwa Idara hiyo.