array(0) { } Radio Maisha | Mwanamme wa umri wa miaka ishirini na mitano achomwa kwa chai moto.

Mwanamme wa umri wa miaka ishirini na mitano achomwa kwa chai moto.

Mwanamme wa umri wa miaka ishirini na mitano achomwa kwa chai moto.

Mwanamme wa umri wa miaka ishirini na mitano anauguza majeraha katika Hospitali ya Rufaa ya Kakamaga baada ya mkewe kumchoma kwa chai moto kufuatia ugomvi kuhusu chakula katika Kijiji cha Umoja-Lugari.

Kwa mujibu wa majirani, mwanamme huyo kwa jina Daniel Omollo alifika nyumbani kwake Alhamisi jioni na kupata mkewe akipika chai. Inaarifiwa alighadhabishwa na mkewe kupika chai ili kunywa kuwa chajio badala ya Ugali.

Majirani wake wanasema alianza kumgombeza mkewe huku akimrushia cheche za maneno, hali ambayo ilimlazimu mkewe Caroline Nekesa kumchoma kwa chai shingoni na kifuani.

Aidha polisi wanasema Nekesa alitoroka baada ya kitendo hicho huku akimwacha mumewe akiuguza majeraha. Majirani baadaye walimpeleka mumewe katika Zahanati ya Lugari Forest ambapo alipewa huduma za kwanza kabla kuhamishwa hadi Hospitali ya Rufaa ya Kakamega.

Chifu wa eneo hilo, Evans Adavaji amesema mshukiwa angali anatafutwa na atakapopatikana atafikishwa mahakamani.