array(0) { } Radio Maisha | Mwanamke anyofolewa macho Eldama Ravine.

Mwanamke anyofolewa macho Eldama Ravine.

Mwanamke anyofolewa macho Eldama Ravine.

Mwanamke mmoja katika eneo la Eldama Ravine ameachwa na majeraha mabaya baada ya watu wasiojulikana kuyanyofoa macho yake.

Inaarifiwa mwathiriwa mwenye umri wa miaka thelathini alifikishwa katika hsopitali ya Nkauru ambapo madaktari walimwarifu kwamba hatakuwa na uwezo wa kuona tena.

Madaktari wa macho wakiongozwa na Benjamin Kariuki wamemwarifu Norah Jepchirchir kwamba kitendo hicho kiliyaathiri macho yote.

Inaarifiwa Jepchirchir alivamiwa na watu wasiolijulikana jana usiku alipokuwa akielekea nyumbani mita chache kutoka kituo cha polisi cha Camp David Eldama Ravine.

Maafisa wapolisi wa eneo la Koibatek wamesema wameanzisha uchunguzi kufuatia tukio hilo.