array(0) { } Radio Maisha | Watu zaidi ya hamsini na saba wafariki nchini Tanzania.

Watu zaidi ya hamsini na saba wafariki nchini Tanzania.

Watu zaidi ya hamsini na saba wafariki nchini Tanzania.

Watu zaidi ya hamsini na saba wamefariki nchini Tanzania baada ya gari la kusafirishia mafuta kushika moto kwenye eneo la Masamvu mjini Marogoro.

Kamanda wa Polisi wa Morogoro Wilbroad Mtafungwa amesema wengi wamejeruhiwa vibaya, huku ikiaminika kuwa huenda idadi ya waliofariki ikaongezeka. Wengi wa waliofariki walikuwa wakijaribu kuchota mafuta baada ya lori hilo kuanguka.

Walioshuhudia ajali hiyo wanasema waendesha piki piki ndio walioathirika zaidi kufuatia ajali hiyo.

Mji wa Morogoro ni moja ya njia kuu za malori yanayobeba shehena za mizigo na mafuta kutoka bandari ya Dar es Salaam.

Bado haijafahamika lori hilo lilikuwa linamilikiwa na kampuni gani ya usafirishaji na iwapo lilikuwa likisafiri nje ya Tanzania au la.