array(0) { } Radio Maisha | Wakenya 4 wapata nafasi ya kupata mafunzo Uingereza

Wakenya 4 wapata nafasi ya kupata mafunzo Uingereza

Wakenya 4 wapata nafasi ya kupata mafunzo Uingereza

Baraza la Uingereza British Council limekamilisha awamu ya tatu ya kuwachagua vijana wanne watakaoenda Uingereza kupata mafunzo chini ya mradi wa Future Leaders Connect.

Zaidi ya vijana 15,000 kutoka mataifa kumi na mawili waliwasilisha stakabadhi zao 1,300 miongoni mwao wakiwa ni Wakenya ila ni wanne tu waliochaguliwa.

Wanne hao - Sharon Adhiambo, Nafula Wafula,Phyllis M. Maina na Alphaxard Gitau watapata mafunzo katika Chuo Kikuu cha Cambridge cha Moller Institute, vilevile kupata nafasi ya kukutana na wabunge na viongozi tajika wa Uingereza.

Washindi wa hapo awali walipata nafasi ya kukutana na waliokuwa Makatibu wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan na Ban Ki-Moon.

Mmoja wa washindi wa awali - Dakta Stellah Bosire ameeleza umuhimu wa mradi huo akisema ulimsaidia pakubwa na kujifunza mengi alipokwenda Uingereza.

Mwaka huu mataifa yaliyoshiriki ni Kenya, Nigeria, Misri, Morocco, Tunisia, Canada, India, Indonesia, Mexico, Pakistan, Poland, Marekani, Uingereza, Wales, Scotland na Ireland Kaskazini.