array(0) { } Radio Maisha | Mzozo wa fedha baina ya Wabunge na Maseneta waathiri huduma za afya

Mzozo wa fedha baina ya Wabunge na Maseneta waathiri huduma za afya

Mzozo wa fedha baina ya Wabunge na Maseneta waathiri huduma za afya

Huku vuta n'kuvute ikiendelea baina ya Magavana na Bunge la Kitaifa, kuhusu mgao wa fedha shughuli za matibabu huenda zikatatizika hata zaidi kwenye hospitali za umma kwenye kaunti kadhaa nchini kuanzia wiki ijayo. Hali hii ni baada ya maafisa mbalimbali wa afya kutoa ilani ya mgomo. Maafisa hao wakiwamo wale wa kliniki na wanafamasia wamesema watawashinikiza wanachama wao kuanza mgomo wiki ijayo iwapo hawatalipwa mishahara yao.

Wakiwahutubia wanahabari jijini Nairobi wamesema mvutano baiana ya bunge, na serikali za kaunti umewaathiri pakubwa. Peterson Wachira ni Mwenyekiti wa Chama cha Kitaifa cha Maafisa wa Kliniki.

Maafisa hao aidha wanashinikiza kubuniwa kwa Tume ya Huduma za Afya kushughulikia masuala ya sekta ya afya ambayo imeendelea kudorora kutokana na usimamizi mbovu. Wamezilaumu serikali za kaunti kwa kushinwa katika jukumu la kuimarisha sekta hiyo huku wakipendekeza usimamizi wake urejeshwe katika serikali kuu.

Hayo yanajiri huku kaunti kumi na mbili miongoni mwa arubaini na saba tayari zikiwa zimewalipa mishahara wafanyakazi wake. Kaunti hizo ni Garissa, Nairobi, Kajiado, Kimabu, Mandera na Tana River. Nyingine ni Turkana, Wajir, Kwale, Bungoma, Kisii na Kakamega.

Mapema wiki hii Muungano wa Wafanyakazi wa serikali za Kaunti ulitoa ilani ya siku saba kwa serikali hizo kuwalipa mishahara yao ya mwezi Julai la si hivyo wagome.