array(0) { } Radio Maisha | Mombasa kukumbwa na uhaba wa maji safi
Mombasa kukumbwa na uhaba wa maji safi

Baadhi ya sehemu kwenye Kaunti ya Mombasa zinatarajiwa kukubwa na uhaba wa maji safi ya matumizi kufuatia  hitilafu za nguvu za umeme kwenye Kituo cha kikuu cha Usambazaji maji cha Baricho.

Katika taarifa kwa vyombo vya habari Mkurugenzi wa mawasiliano kwenye serikali ya Kaunti hiyo Richard Chacha amesema kwamba hatua hiyo imeathiri usambazaji wa maji hadi kwenye Kituo maalum cha Nguu tatu ambacho husambaza maji kwenye maeneo mbalimbali ya Jiji la Mombasa.

Maeneo ya Kisiwani Mombasa, Shanzu, Bamburi, Nyali, Mtopanga, Kongowea, Kisimani, Kisauni na Mishomoroni yameathiriwa na hali hiyo.

Chacha hata hivyo amesema tayari wataalam pamoja na mafisa wa Kampuni ya Kusambaza Umeme Kenya Power wametumwa ili kuhakikisha hali ya kawaida inarejea.