array(0) { } Radio Maisha | Museveni, magufuli Tshisekedi, watarajiwa kuhudhuria uzinduzi Kisumu

Museveni, magufuli Tshisekedi, watarajiwa kuhudhuria uzinduzi Kisumu

Museveni, magufuli Tshisekedi, watarajiwa kuhudhuria uzinduzi Kisumu

Rais Uhuru Kenyatta atawaongoza marais Yoweri Museveni wa Uganda, Felix Tshisekedi wa Jumahuri ya Kidemokrasi ya Congo na John Magufuli wa Tanzania katika uzinduzi wa mradi wa Bandari ya Kisumu, mradi mkubwa zaidi katika eneo la Magharibu ya nchini uliogharimu shilingi bilioni 3.

Aidha, inaarifiwa kwamba Mjumbe Maalumu wa Ujenzi wa Miundo msingi Barani Afrika, Raila Odinga atakutana na viongozi hao wiki ijayo.

Mapema jana, Msemaji wa Serikali Kanze Dena alisema serikali itatoa mwelekeo zaidi kuhusu uzinduzi wa bandari hiyo wiki ijayo huku Mamlaka ya Bandari Nchini KPA ikiwa imekamilisha ujenzi wa mradi huo.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa KPA Daniel Manduku, bandari hiyo itatoa nafasi kati ya 100 na 200 za ajira moja kwa moja baada tu ya kufunguliwa.

KPA inalenga kuifanya bandari hiyo kuwa kitega-uchumi kitakachosaidia shughuli mbalimbali za kibiashara katika maeneo ya Mbita, Homa Bay, Kisiwa cha Mfangango, Muhuri Bay Pier, Ufuo wa Usenge vilevile Bandari ya Ziwa Victoria.

Ikumbukwe tayari Rais Uhuru Kenyatta na Naibu wake, William Ruto walizuru eneo hilo kukagua miradi inayoendelea kuwekezwa na serikali.