array(0) { } Radio Maisha | Shirika la Standard Group laahidi kuendelea kukuza vipaji

Shirika la Standard Group laahidi kuendelea kukuza vipaji

Shirika la Standard Group laahidi kuendelea kukuza vipaji

Shirika la Habari la Standard PLC limeahidi kuendelea na mipango yake ya kukuza vipaji, vilevile kuwawezesha vijana kujiendeleza. Afisa Mkuu Mtendaji wa shirika hili, Orlando Lyomu amesema licha ya changamoto, zipo fursa nyingi za vijana kujiendeleza na kusema ni sharti watie bidii ili kupiga hatua hata zaidi.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa awamu ya tatu ya mpango wa kutoa mafunzo ya uanahabari kwa wanafunzi waliohitimu kutoka vyo vikuu kupitia taasisi ya Standard Group Academy katika Chuo Kikuu cha Aga Khan, Lyomu aidha amewashauri vijana wazingatie uandishi mzuri wa taarifa na kuwa na mazoea ya kusoma machapisho mbalimbali na kujifunza mambo mengi ili kujiboresha katika taaluma ya uanahabari.

Mpango huu unatekelezwa kwa ushirikiano baina ya Standard na Chuo Kikuu cha Aga Khan.