array(0) { } Radio Maisha | Bunge linapendekeza majeshi kutumwa kuulinda mpaka unaozozaniwa baina ya Kenya na Somalia

Bunge linapendekeza majeshi kutumwa kuulinda mpaka unaozozaniwa baina ya Kenya na Somalia

Bunge linapendekeza majeshi kutumwa kuulinda mpaka unaozozaniwa baina ya Kenya na Somalia

Wabunge sasa wanataka majeshi ya Kenya kutumwa kulinda mpaka baina ya Kenya na Somalia kufuatia eneo linaozonaniwa baina ya mataifa haya mawili. Kiongozi wa Wengi katika Bunge la Kitaifa Adan Duale na Mwenzake wa Wachache John Mbadi wamewasilisha hoja bungeni kuhusu suala hilo.

Mswada huo unasemekana kuchochewa na hatua ya Somalia kufutilia mbali mchoro wa ramani wa mwaka 19964. Somalia inashikilia kwamba mchoro wa Kenya  unachorwa kuelekea kusini mashariki kufika majini huku Kenya nayo ikisisitiza kwamba mchoro wake unachorwa kuelekea mashariki.

Akiuwasilisha hoja hiyo, Duale amewashauri wabunge kuipitisha itakapowasilishwa tena kwa mjadala,akisema ni wajibu wa serikali kuilinda mipaka yake kwa mujibu wa katiba. Aidha katika hoja hiyo Duala na Mbadi wanataka mzozo huo kusuluhishwa kwa njia ya kidiplomasia nchini ya uongozi wa Umoja wa Afrika AU, Mamlaka ya Kimataifa ya Maendeleo IGAD na Muungano wa Matiafa ya Afrika Mashariki. Wanapinga kuhusishwa kwa Mahakama ya Kimataifa ya Haki ICJ katika suala hilo.

Kesi baina ya Kenya na Somali kuhusu sehemu hiyo,  inatarajiwa kuanza Septemba tarehe 9 katika mahakama ya ICJ nchini Uholanzi.  Hayo yanajiri huku kukiwa na kesi katika Mahakama Kuu nchini,  inayolenga kuizuia Kenya kushiriki katika kesi hiyo.

Mzozo ulianza mapema mwaka huu, baada ya Somalia kunadi baadhi ya visima vya mafuta na gesi kwenye eneo linalozozaniwa, kwa kampuni kutoka mataifa ya Uingereza , Ireland Kaskazini na Norway. Sehemu inayozaniwa ni takribani kilomita mia moja mraba katika Bahari Hindi.

Ikumbukwe Wabunge wataanza likizo yao leo hii ila Karani wa Bunge la Kitaifa Miachael Sialai amesema amjadala kuhusu suala hilo utafanyika punde bunge litakaporejelea vikao.