array(0) { } Radio Maisha | Polisi wamemuua mshukia wa uvamizi katika eneo la Kisauni, Mombasa

Polisi wamemuua mshukia wa uvamizi katika eneo la Kisauni, Mombasa

Polisi wamemuua mshukia wa uvamizi katika eneo la Kisauni, Mombasa

Polisi katika eneo la Kisauni kwenye Kaunti ya Mombasa wamefanikiwa kumuua kwa kumpiga risasi kijana mmoja mwanachama wa genge la uhalifu usiku wa kuamkia leo.

Kamanda wa Polisi eneo hilo Julius Kiragu alisema kwamba mshukiwa huyo na wenzake wawili waliofanikiwa kutoroka walipatikana wamejihami kwa panga eneo la Mtopanga tayari kufanya uvamizi.

Maafisa wa polisi waliokuwa wakishika doria waliwaamrisha kujisalimisha na wakakaidi amri na kuanza kuwashambulia ndiposa akauliwa huku wenzake wakitoroka. Inakisiwa kwamba watatu hao ni miongomi mwa genge la vijana lililowavamia watu siku tatu zilizopita eneo la Bamburi na kuwajerihi vibaya kumi na mmoja.

Msako dhidi ya wawili ambao wako mafichoni unaendelea huku mwili wa aliyeuliwa ukiwa umelazwa katika hifadhi ya maiti ya hospitali ya Rufaa ya Coast General Jijini Mombasa.

Vijana wanne wanaoshukiwa kuwa miongoni mwa genge lililotekeleza uvamizi huo walitiwa mbaroni na polisi wamekuwa wakiendelea kuwatafuta washukiwa wengine sita ambao wamekuwa mafichoni. John Elungata ni mshirikishi wa utawala katika eneo la Pwani.

Ikumbukwe polisi wanachunguza iwapo washukiwa wa uvamizi huo wanahusika kwa vyovyote na shughuli za ulanguzi wa dawa za kulevya ambazo zilinaswa siku chache zilizopita na idara za usalama, katika eneo la Pwani.