array(0) { } Radio Maisha | Wakenya waadhimisha Miaka 21 tangu shambulio la kigaidi jijini Nairobi

Wakenya waadhimisha Miaka 21 tangu shambulio la kigaidi jijini Nairobi

Wakenya waadhimisha Miaka 21 tangu shambulio la kigaidi jijini Nairobi

Wakenya katika mitandao ya kijamii wanaaadhimisha Miaka 21 tangu shambulio la kigaidi lililofanyika katika ubalozi wa Marekani jijini Nairobi na dakika chache baadaye katika ubalozi wa Marekani jijini Dar es Salaam Tanzania.

Katika visa hivyo viwili watu mia mbili ishirini na wanne walifariki dunia, mia mbili thelathini na mmoja nchini Kenya na kumi na mmoja Jijini Dar es Salaam, huku zaidi ya watu 5,000 wakijeruhiwa.

Ubalozi wa Marekani Nchini kupitia mtandao wa twitter umeadhimisha siku hii kwa kuwakumbuka waliofariki na waliojeruhiwa nikinukuu sehemu ya ujumbe huo." . . . you are in our hearts, minds, and prayers. we are united, Americans and Kenyans."