array(0) { } Radio Maisha | Wako wapi madaktari wa Cuba waliotekwa nyara.
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Wako wapi madaktari wa Cuba waliotekwa nyara.

Wako wapi madaktari wa Cuba waliotekwa nyara.

Kwa mara ya kwanza baada ya miezi kadhaa, Inspekta Mkuu wa Polisi Hilary Mutyambai amelizungumzia suala la madaktari wawili raia wa Cuba waliotekwa nyara kwenye Kaunti ya Mandera miezi miine iliyopita.

Mutyambai amesema kwamba serikali kwa ushirikiano na taasisi nyinginezo za kimataifa inaendeleza juhudi za kuwaokoa Assel Herera Corea na Landy Rodriguez waliotekwa nyara mwezi Aprili mwaka huu na kundi la Al Shabaab wakati waliposhambuliwa wakielekea kazini.

Aidha, Mutyambai amefafanua changamoto zinazowakumba maafisa wa polisi waliojukumiwa kutekeleza oparesheni ya kuwaokoa wawili hao akisema kwamba sheria za kimataifa haziwaruhusu kutekeleza oparesheni za kiusalama katika taifa geni.

Uchunguzi wa hivi karibuni umebainisha kwamba raia hao wa Cuba walihamishwa hadi msitu wa Halaanqo karibu na mji wa Barawe ambako inaarifiwa tayari wamejiunga na dini ya kiislamu.

Wakati wa shambulio hilo, afisa mmoja wa polisi aliyekuwa ndani ya gari lao aliuliwa huku mwenzake akijeruhiwa.

Kundi hilo la kigaidi baadae lilidai kikomboza cha shilingi milioni 150, kwa mujibu wa baraza la wazee lililotumwa kushiriki mazungumzo na kundi hilo katika Kijiji cha Jubbaland, Somalia.