array(0) { } Radio Maisha | Familia ya Okoth yajitenga na wito wa Wazee.

Familia ya Okoth yajitenga na wito wa Wazee.

Familia ya Okoth yajitenga na wito wa Wazee.

Familia ya aliyekuwa Mbunge wa Kibra Ken Okoth imejitenga na wito wa wazee wa jamii ya Waluo kwenye eneo la Kabondo Kasipuli Kaunti ya Homa Bay kwamba sharti mjane wa Okoth, Monicah Lavenda afanyiwe tambiko kabla kurithiwa.

Kwa mujibu wa mamaye Okoth, Angelina Ongera, wataandaa ibada ya maombi katika eneo hilo ili kumpa heshima mwendazake badala ya kuuzika mgomba. Aidha, Mbunge wa eneo hilo Eve Obara amesema viongozi wa ODM watahudhuria ibada hiyo.

Hata hivyo, mzee wa jamii, Apollo Bwana amesisitiza kwamba sharti mgomba wa ndizi uzikwe kulingana na mila na desturi za jamii hiyo.

Wakati uo huo, ODM imejitenga na madai kwamba iliongozwa kuteketezwa kwa mwili wa Okoth Jumamosi wiki iliyopita. John Mbadi ni Mwenyekiti wa chama hicho.