array(0) { } Radio Maisha | Sarakasi imeshuhudiwa katika kikao cha Seneti iliyofanywa kwa lugha ya kiswa

Sarakasi imeshuhudiwa katika kikao cha Seneti iliyofanywa kwa lugha ya kiswa

Sarakasi imeshuhudiwa katika kikao cha Seneti iliyofanywa kwa lugha ya kiswa

 

Sarakasi imeshuhudiwa katika kikao cha alasiri cha Bunge la Seneti wakati maseneta walipokuwa wakichangia mijadala katika lugha ya Kiswahili. Utata hasa ulishuhudiwa wakati Seneta Maalum, Agnes Zani aliposimama kuchangia mjadala na kutumia neno *Mzungumzishi kumaanisha Spika. Suala hilo liliiibua mjadala kwa takriban saa nzima huku maseneta wakitofautiana kuhusu usahihi wake. 

Neno hili lilotumiwa na Seneta Agnes Zani ambalo lilibua mjadala mkali bungeni huku maseneta wakitaka kufahamu kuhusu usahihi wake. Aliyekuwa wa kwanza kulikosoa ni Seneta wa Kaunti ya Narok, Ledama Ole Kina ambaye naye awali alilazimika kusitisha mchango wake kwa lugha ya Kiswahili kwa kukosa ufasaha.

Hata hivyo, maji yalizidi unga huku maseneta wengine mfano Cleophas Malala wakilazimika kutumia mtandao kubainisha iwapo neno hilo linakubalika katika Kiswahili..

 

 

Ikamlazimu Spika, Kenenth Lusaka kuamuru kusitishwa kwa utumiaji wa neno hilo hadi suala hilo litakapojadiliwa kwa kina katika kikao kingine huku Zani akiendelea kulitumia,

Hatimaye, Spika Lusaka alilazimika kumfursha Zani bungeni kwa kukiuka maagizo yake na kukataa kuomba msamaha..