array(0) { } Radio Maisha | Serikali imekana mipango ya kuagiza mahindi kutoka taifa la Mexico,
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

Serikali imekana mipango ya kuagiza mahindi kutoka taifa la Mexico,

Serikali imekana mipango ya kuagiza mahindi kutoka taifa la Mexico,

Serikali imesema itaagiza mahindi kutoka mataifa jirani na yale ambayo ni wanachama wa Muungano wa COMESA pekee wala sio Mexico inavyodaiwa. Akihojiwa mbele ya Kamati ya Kilimo Bugeni,Waziri wa Kilimo Kiunjuri aidha ameutetea mpango wa serikali wa kuagiza mahindi kutoka mataifa mengine huku akisema unalenga kukabili upungufu wa bidhaa hiyo muhimu siku za usoni. Kiunjuri aidha amesema licha ya madai ya kuwapo wa mahindi ya kutosha nchini, mahindi magunia milioni sita yanahitajika ili kukabili kuongezeka kwa bei ya unga, ambao sasa unauzwa kwa shilingi mia moja ishirini kwa paketi ya kilo mbili.

Waziri huyo aida ametakiwa kuelezea alikotoa pesa za kulipia fedha kwa kampuni ya Commodity House ilhali fedha hizo hazikuwa zimetengwa katika bajeti. Kiunjuri amejitetea na kusema kwamba kampuni hiyo ni miongoni mwa zinazoidai wzara yake fedha na wala haikukieka sheria wakati wa malipo.

Awali viongozi wa eneo la Bonde la Ufa wameendelea kumshinikiza  Kiunjuri pamoja na katibu wa wizara yake kujiuzulu kuhusu pendekezo lao kuishinikiza serikali kuagiza mahindi kutoka mataifa ya nje.

Wakiongozwa na Mbunge wa Cheranganyi Joshua Kutunyi, viongozi hao wamemlaumu kwa kuwalipa mawakala wa uuzaji mahindi ilhali kuna mahindi ya kutosha humu nchini. Kutunyi aidha amedai kuwa fedha zilizotengwa na serikali kununua mahindi kutoka kwa wakulima huenda zikaibwa na watu wachache huku akisema Waziri Kiunjuri alipuuza ushauri uliotolewa na Shirika la Uhifadhi wa Chakula.

Mbunge huyo vilevile, anataka baadhi ya kampuni na wafanyabiashara waliolipwa bila sheria kufuatwa kuchunguzwa akisema hali hiyo imechangia kulipwa kwa matapeli bila kuzingatia sheria. 


Kwa upande wake mbunge wa saboti Caleb Khamis amesema kwamba hatasalia kimya wakati ambapo kilimo kinaendelea kusambaratishwa na wakulima kuumia. Akiunga mkono shinikizo la Waziri kujiuzulu, Khamis anataka wizara nzima ya kilimo kufanyiwa mabadiliko.