array(0) { } Radio Maisha | Mshukiwa wa ulawiti aachiliwa kwa dhamana ya shilingi alfu 50 na mahakama ya Shanzu

Mshukiwa wa ulawiti aachiliwa kwa dhamana ya shilingi alfu 50 na mahakama ya Shanzu

Mshukiwa wa ulawiti aachiliwa kwa dhamana ya shilingi alfu 50 na mahakama ya Shanzu

Mahakama ya Shanzu imemwachilia kwa dhamana ya shilingi elfu hamsini mhudumu wa teksi aliyekamatwa jana kwa madai ya kumlawiti mvulana mwenye umri wa miaka kumi na mitatu.

Fredrick Njenga Mungai aliyekamatwa kwa madai ya kumshurutisha mvulana huyo ambaye ni mwanafunzi wa Shule ya Msingi ya Light Academy iliyo katika eneo la Nyali kwenye Kaunti ya Mombasa kumgusa sehemu za siri hata hivyo hajaruhusiwa kujibu mashtaka.

Hakimu Mkuu, Yusuf Shikanda ameuagiza upande wa mashtaka kuwasilisha kesi hiyo upya kwa msingi kwamba mashtaka yaliyowasilishwa mbele ya mahakama hiyo yalikuwa na dosari.

Kesi hiyo inatarajiwa kuwasilishwa upya tarehe ishirini na tatu mwezi huu. Kulingana na taarifa iliyonakiliwa katika Kituo cha Polisi cha Nyali, mhudumu huyo alipigiwa simu Jumatatu jioni kumchukua mwanafunzi huyo ambaye ni wa darasa la nane ili kumsafirisha hadi nyumbani kwao. Taarifa hiyo aidha imebaini kwamba Njenga aliegesha gari hiyo kando ya barabara mita chache kabla kufika nyumbani kwa mtoto huyo kisha kumfanyia kitendo hicho.