array(0) { } Radio Maisha | Rais Uhuru Kenyatta amesifia hatua ambazo taifa limepiga katika sekta ya biashara

Rais Uhuru Kenyatta amesifia hatua ambazo taifa limepiga katika sekta ya biashara

Rais Uhuru Kenyatta amesifia hatua ambazo taifa limepiga katika sekta ya biashara

Rais Uhuru Kenyatta  amesifia hatua ambazo  taifa limepiga katika sekta ya biashara na kutoa mazingira mazuri kwa wawekezaji 

Akizungumza katika ufunguzi wa sherehe za 21 za Jumuiya ya Mataifa ya Afrika Mashariki na Kusini COMESA, Kenyatta amesema kwamba Kenya itaendelea kushirikiana kibiashara na matiafa ya kigeni kuinua uchumi wa nchi.


Rais amewahimiza wanachama wa COMESA kutilia maanani ukuaji wa uchumi wa mataifa yao kupitia biashara ili kuimarisha maisha ya wananchi.

Kenyatta aidha  amewataka wanachama hao kuweka mikakati mbalimbali ya kuboresha ushirikiano wa kibiashara na kutoa nafasi za ajira kwa idadi kubwa ya  vijana ambao wamekamilisha masomo ilhali hawana nafasi za kazi.


Rais wa Uganda Yoweri Museveni kwa upande wake amewataka wanachama hao kutangamana kibiashara na kufuata mtindo wa Uchina ambayo licha ya kuwa na soko kubwa inaendelea kutafuta masoko nje ya mipaka yake.