array(0) { } Radio Maisha | Wafanyabiashara jijini Nairobi wapewa wiki moja kuyapaka rangi nyamba za biashara

Wafanyabiashara jijini Nairobi wapewa wiki moja kuyapaka rangi nyamba za biashara

Wafanyabiashara jijini Nairobi wapewa wiki moja kuyapaka rangi nyamba za biashara

Serikali ya Kaunti ya Nairobi imetoa makataa ya wiki moja kwa wamiliki wa nyumba za biashara katikati ya jiji la Nairobi, kuyapaka rangi ama wachukuliwe hatua za kisheria ikiwa njia mojawapo ya kuboresha sura ya jiji.

Gavana wa Nairobi Mike Sonko, ametoa agizo hilo akisema litahakikisha kwamba jiji la Nairobi linawavutia wawakezaji na kuboresha shughuli za kibiashara nchini.

Sonko aidha amesema kwamba hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi ya wafanyabiashara ambao hawatakuwa wamezingatia mwongozo  huo kufikia mwisho wa makataa hayo.

Agizo hilo linawajumuisha wenye biashara katika maeneo ya Barabara ya Uhuru, Mto Nairobi, Ring Road ,Pumwani na Haile Salassie.

Mwaka wa 2017, jiji la Nairobi liliorodheswa ya pili miongoni mwa miji 20 mikuu  za Afrika yenye ukuaji kasi wa shughuli za kibiashara na uchumi.