array(0) { } Radio Maisha | Mahakama imeondoa agizo la kukamatwa kwa mchezaji wa raga, Alex Mahaga Olaba anayehusishwa na madai ya ubakaji

Mahakama imeondoa agizo la kukamatwa kwa mchezaji wa raga, Alex Mahaga Olaba anayehusishwa na madai ya ubakaji

Mahakama imeondoa agizo la kukamatwa kwa mchezaji wa raga, Alex Mahaga Olaba anayehusishwa na madai ya ubakaji

Mahakama moja ya Nairobi imeondolea mbali agizo la kukamatwa kwa mchezaji wa raga, Alex Mahaga Olaba baada ya kujiwasilisha mahakamani leo hii.

Hakimu Mkuu, Martha Mutuku ameliondoa agizo hilo baada ya kuyakubali maelezo yaliyotolewa na mchezaji huyo ya kukosa kufika mahakamani mara mbili mfululizo wiki iliyopita akisema alikuwa akiugua. Aidha, Hakimu Mutuku amesema Olaba alihudhuria vikao vya kesi dhidi yake mbeleni bila kukosa.

Olaba ameshtakiwa pamoja na mchezaji mwingine, Lawrence Frank Wanyama kwa madai ya kumbaka kwa zamu mwanamke mmoja mnamo Februari 11 mwaka 2018 katika jengo la Seefa mtaani Highrise, jijini Nairobi wakati walipokuwa wakihudhuria sherehe.

Washtakiwa waliachiliwa kwa dhamana ya shilingi laki tano pesa taslimu kila mmoja. Tayari walijitetea kwamba mwanamke huyo alishiriki mapenzi nao kwa hiari.