array(0) { } Radio Maisha | Gavana wa Kiambu Ferdinand Waitutu mkewe Susan Wangari na mwanao Monicah Njeri wanatarajiwa kushtakiwa kwa makosa ya ufisadi

Gavana wa Kiambu Ferdinand Waitutu mkewe Susan Wangari na mwanao Monicah Njeri wanatarajiwa kushtakiwa kwa makosa ya ufisadi

Gavana wa Kiambu Ferdinand Waitutu mkewe Susan Wangari na mwanao Monicah Njeri wanatarajiwa kushtakiwa kwa makosa ya ufisadi

Gavana wa Kiambu Ferdunad Waitutu mkewe Susan Wangari na mwanao Monicah Njeri wanatarajiwa  kushtakiwa kwa makosa ya ufisadi. 

Tayari Tume ya Maadili na Kukabili Ufisadi EACC imependekeza washtakiwe kwa matumizi mabaya ya mamlaka katika utoaji wa tenda ya shilingi milioni 588 na ununuani wa jumba kwa gharama ya shilingi milioni 221.

Maafisa wengine  kadhaa wa kaunti vilevile wanachunguzwa wakiwamo wanachama wa kamati ya tenda, Afisa wa Barabara Lucas Waihinya, wakurugenzi wa Kampuni za M/S Testimony  Enterprises iliyopewa tenda ya kujenga barabara.

Gavana Waititu analaumiwa kwa  kupokea fedha  za tenda kadhaa kupitia akaunti zake za mkewe na mwanao kadhalika kutolewa kwa tenda katika  maeneo ya Limuru, Thika, Gatundu, Juja na Ruiru pasi na kufuatwa kwa utaratibu. Kwa mfano shilingi milioni 25.4 zimesekana kulipwa kulipwa kwa kauanti ya Waititu zikiwa ni sehemu ya  fedha ziliozofaa kulipiwa mradi wa barabara Ikumbukwe.

Waititu alitiwa mbaroni mwezi Mei mwaka huu kabla ya kuachiliwa kwa dhamana ya shilingi  elfu mia tano. Tayari Mkuu wa Mashtaka, Noordin Hajj ameidhinisha baadhi ya mashtaka.