array(0) { } Radio Maisha | Mswada wa Ugavi wa Mapato wa mwaka 2019 umechapishwa na unatarajiwa kuwasilishwa bungeni juma lijalo

Mswada wa Ugavi wa Mapato wa mwaka 2019 umechapishwa na unatarajiwa kuwasilishwa bungeni juma lijalo

Mswada wa Ugavi wa Mapato wa mwaka 2019 umechapishwa na unatarajiwa kuwasilishwa bungeni juma lijalo

Mswada wa Ugavi wa Mapato wa mwaka 2019 umechapishwa na unatarajiwa kuwasilishwa katika Bunge la Kitaifa Jumanne wiki ijayo wakati wabunge watakaporejelea vikao vyao baada ya likizo fupi.

Mswada huo una pendekeza kima cha shilingi bilioni 316 kugawanywa kwa serikali za kaunti 47 japo upo uwezekano mkubwa wa kiwango hicho cha fedha kupingwa na Bunge la Seneti.

Tayari Baraza la Magavana limepinga pendekezo hilo. Kupitia taarifa kwa vyombo vya habari, Mwenyekiti wa Baraza hilo ambaye pia ni Gavana wa Kakamega Wycliffe Oparanya amepinga kiwango hicho cha shilingi bilioni 316 na kusisitiza kwamba sharti serikali za kaunti zitengewe shilingi bilioni 335 jinsi ilivyopendekezwa na Tume ya Ugavi wa Mapato.

Aidha, Baraza hilo limesema litasubiri uamuzi wa Mahakama ya Juu tarehe 19 mwezi huu kuhusu suala hilo.

Ikumbukwe kuwa mswada wa awali ambao ulipendekeza serikali za kaunti kutengezea shilingi bilioni 310 uliangushwa bungeni baada ya Bunge la Kitaifa na lile la Seneti kukosa kuafikiana kuhusu kiwango hicho.

Kiongozi wa Wengi katika Bunge la Kitaifa Aden Duale aliilaumu Tume ya Ugavi wa Mapato kwa kile alichokitaja kuwa kuwapa magavana matumaini kwamba kiwango cha fedha wanachopendekeza kitaafikiwa na hivyo kulemaza shughuli kwenye kaunti mbalimbali.