array(0) { } Radio Maisha | Polisi wawili na dereva wa Naibu Gavana wa Homabay waachiliwa kwa dhamana

Polisi wawili na dereva wa Naibu Gavana wa Homabay waachiliwa kwa dhamana

Polisi wawili na dereva wa Naibu Gavana wa Homabay waachiliwa kwa dhamana

Maafisa wawili wa polisi na dereva wa Naibu Gavana wa Homabay, Hamilton Orata walioshtakiwa kwa madai ya mauaji wameachiliwa huru kwa dhamana ya shilingi laki tano kila mmoja na mdhamini wa kiasi sawa na hicho.

Maafisa hao Fredrick Kimanzi na Lawi Gitari pamoja na dereva kwa jina Alex Onyango, walikamatwa wiki iliyopita kwa madai ya kumuua   Abdinasir Ahmed.

Wanadaiwa kutekeleza mauaji hayo kati ya April 27 na 28 mwaka huu katika hoteli moja mjini Ndhiwa. Hata hivyo wamekana mashtaka dhidi yao mbele ya Jaji Joseph Karanya wa Mahakama Kuu ya Homa Bay.

Kesi hiyo itasikilizwa Novemba 4 mwaka huu.