array(0) { } Radio Maisha | Rais Uhuru Kenyatta anatarajiwa kulifungua rasmi Kongamano la Kibiashara la COMESA.

Rais Uhuru Kenyatta anatarajiwa kulifungua rasmi Kongamano la Kibiashara la COMESA.

Rais Uhuru Kenyatta anatarajiwa kulifungua rasmi Kongamano la Kibiashara la COMESA.

Rais Uhuru Kenyatta anatarajiwa kulifungua rasmi Kongamano la Kibiashara la 21 la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kusini, COMESA Jumatano wiki hii hapa jijini Nairobi.

Msemaji wa Ikulu, Kanze Dena amesema kongamano hilo linaashiria kwamba taifa linaendelea kukua kiuchumi hivyo kuvutia wawekezaji wengi humu nchini.

Msemaji huyo aidha amesema Rais Uhuru Kenyatta atazuru Kaunti ya Turkana ili kuzundia Kiwanda cha Kawi, ambacho ndicho kiwanda kikubwa zaidi Barani Afrika.  Kiwanda hicho kina tabo za umeme 365 zenye uwezo wa kuzalisha kilowati 850 kwa kawi kila mmoja.

Aidha Kanze amedokeza kwamba wiki ijayo Rais wa Botswana, Erick Masisi atakuwa nchini kwa ziara ya kiserikali.